Kuchokonoa Mzinga wa Nyuki
"Kuchokonoa Mzinga wa Nyuki" ni simulizi iliyoandikwa na Arai Ran. Inahusu mtaalam wa wadudu aitwaye F. Aliyewahi kuwa mwanafunzi mwenzake katika chuo kikuu anamtambulisha kwa E, mgonjwa asiye wa kawaida. Nyuki wamejenga mzinga kwenye tumbo la E. F anashangaa lakini shauku yake kama mtafiti imeshika kasi na anaamua kumchukua E. Kisha anafuatilia hali hiyo. Hatima ya kushangaza inamsubiri.