Riwaya - Jua: sehemu 2
Kahara anaugua "maumivu mbadala" makali ya jino yanayosababishwa na maumivu ya moyo. Daktari Kazama wa zahanati ya ajabu anamwambia atasumbuliwa na maumivu hayo hadi atakapofahamu sababu ya kweli ya maumivu yake ya moyo. Kahara anashuku inaweza kuwa aliyewahi kuwa mpenzi wake, aliyechepuka na kumwacha. Pia anafikiria kufungwa kwa baa yake pendwa, kelele za kuudhi za jirani yake na matatizo na mkuu wake wa kazi. Pengine mkusanyiko wa hayo yote ndio unamwelemea. Kahara ataweza kubaini chanzo hasa cha maumivu yake?