Riwaya - Jua: sehemu 1
Usiku, ilipotangazwa hali ya dharura Japani, Kahara anajikuta akielemewa na maumivu ya jino. Hawezi kuweka miadi kwa daktari wa meno popote na hatimaye anafika kwenye zahanati ya ajabu ya meno isiyo na tovuti, maoni wala dalili za wagonjwa wengine. Kazama, mkurugenzi wa zahanati hiyo anamwambia kuwa ana "maumivu mbadala" yanayosababishwa na maumivu ya moyo. Kahara anatakiwa kubaini sababu ya kweli ya maumivu yake na hivyo anasimulia hisia zake. Anashuku inaweza kuwa aliyewahi kuwa mpenzi wake, aliyechepuka na kumwacha hivi karibuni.