"Mama Yangu ni Mwandishi wa Blogu Aliyefanikiwa": Sehemu 2
Natsu anagundua kuwa mama yake ni mwandishi wa blogu maarufu inayohusu mapishi yake. Anajikuta akiifuatilia blogu hiyo na kuishia kuandika maoni bila kutaja jina lake. Blogu hiyo inafichua pande mpya za mama yake asiyezungumza sana. Lakini bado, Natsu anasita kumuuliza moja kwa moja juu ya blogu hiyo. Kisha, Natsu anahamishiwa Tokyo kikazi. Anahama ijapokuwa ana wasiwasi kumwacha mama yake peke yake. Katika hali hiyo, blogu ya mama yake inaanza kubadilika....Hii ni sehemu ya pili ya simulizi ya kusisimua kuhusu mama na bintiye kama inavyohadithiwa kupitia mapishi na blogu.