"Mama Yangu ni Mwandishi wa Blogu Aliyefanikiwa": Sehemu 1
Siamini! Mama yangu ni mwandishi wa blogu mwenye wafuasi wengi! Natsu ni mfanyakazi wa ofisini anayegundua blogu inayohusu mapishi inayoandikwa na mama yake. Ni blogu maarufu yenye makumi ya maelfu ya wafuasi. Natsu hawasiliani vizuri na mama yake na anashindwa kumuuliza juu ya blogu hiyo, ambayo kwa yeye inajadili maisha yake pia. Lakini uhusiano wao unabadilika baada ya Natsu kuandika maoni kwenye blogu hiyo. Hii ni sehemu ya kwanza ya simulizi ya kusisimua kuhusu mama na bintiye kama inavyohadithiwa kupitia mapishi na blogu.