Riwaya - Huwezi Ukaiona: Sehemu 2
Etsuro anatembea kuelekea nyumbani huku mvua ikinyesha akiambatana na mwanamume mzee aliyekutana naye kwenye kituo cha treni sehemu ya kusubiria teksi, na mzee huyo anaanza kumzungumzia mbwa wake. Jina la mbwa huyo ni Sita, na siku moja anaanza tu kumfuata binti mmoja. Katika simulizi hii ya ajabu, binti huyo aliota ndoto iliyojirudia kumhusu Sita, lakini hii ilikuwa mara yake ya kwanza kumwona mbwa huyo ana kwa ana. Yeye na Sita wanapendana kwenye hizo ndoto, lakini Sita anafariki mara moja. Etsuro anajikuta akivutiwa mno na kisa hicho cha kutisha. Anadhani ilikuwa ni simulizi ya ajabu tu, ila inaonekana kuna yaliyojificha zaidi. Kwa nini Etsuro anaogopa mno, na huyu mzee ni nani hasa?