Riwaya - Huwezi Ukaiona: Sehemu 1
Miyabe Miyuki ni mmoja wa waandishi mashuhuri zaidi nchini Japani, na kazi yake inajikita kwenye hadithi za mafumbo, za kutisha, sayansi ya kufikirika, riwaya za kihistoria na fasihi ya watoto. Hadithi hii ya kutisha inaanzia usiku wa mvua ambapo mhusika mkuu anakutana na mwanamume mzee wakati akisubiri teksi kwenye kituo cha treni. Etsuro alilikosa basi la mwisho na anasubiri teksi wakati mwanamume huyo mzee aliyekuwa mstarini nyuma yake anaanzisha mazungumzo naye. Mzee huyo anaonekana kuwa mtu mzuri na Etsuro anakubali mwaliko wake wa kutembea pamoja kuelekea nyumbani. Wakati wakitembea kwenye mvua, mzee anaanza kusimulia kisa cha ajabu kuhusu mbwa wake.