Ripoti: Tamasha la Wanafunzi

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu Tamasha la Wanafunzi lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Tokyo likihusisha utamaduni wa mataifa mbalimbali ikiwemo vyakula, muziki na maigizo. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 25, 2023.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 17, 2023.)

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Tokyo wakifanya igizo katika Tamasha la Wanafunzi lililofanyika chuoni hapo.
Radhia Suzuki wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN akifanya mahojiano na wanafunzi walioshiriki Tamasha la Wanafunzi lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Tokyo
Greyson Ishengoma, afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Japani akizungumzia Tamasha la Wanafunzi lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Tokyo.
Baadhi ya matukio katika Tamasha la Wanafunzi lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Tokyo.