Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda ambaye amefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya NHK.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda akiwa katika studio za Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.