Ripoti: Sehemu ya Pili ya Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japani mwaka 2023
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea sehemu ya pili ya ripoti kuhusu Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japani mwaka 2023 yaliyofanyika jijini Osaka kuanzia Oktoba 26 hadi 29.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Afisa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, NCAA akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.
Afisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, TANAPA akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.
Balozi wa Tanzania nchini Japani, Baraka Luvanda (kulia) akiwa na washiriki wengine wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japani mwaka 2023.
Banda la Tanzania katika Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Japani mwaka 2023 jijini Osaka.