Mahojiano: Bongo Zozo
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Bongo Zozo, ambaye ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii kuhusu ziara yake nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Bongo Zozo akiwa na mtangazaji Mbozi Katala katika studio za Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.
Bongo Zozo akiwa na mtangazaji Mbozi Katala alipoitembelea Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.