Mahojiano: Erick Mfugale na Bongo Zozo
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Erick Mfugale, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania ambaye amekuja nchini Japani mjini Nagai mkoani Yamagata lakini pia tutakuletea sehemu ya kwanza ya mahojiano na Bongo Zozo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 5, 2023.)
Erick Mfugale / Bongo Zozo
Erick Mfugale akiwa na wanariadha wa Tanzania walioshiriki mbio za Nagai Marathon.
Erick Mfugale akiwa na wanariadha wa Tanzania pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda na maafisa wengine baada ya kumalizika kwa mbio za Nagai Marathon.