Mahojiano: Martin Mwanje na Semi za Kijapani
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Martin Mwanje kuhusu mkutano kati ya Rais William Ruto wa Kenya na Balozi wa Japani nchini Kenya, Okaniwa Ken uliofanyika ikulu ya Nairobi, pia tunakuletea kipindi cha Semi za Kijapani na nahau ya leo ni "Oya no Sune o Kajiru."

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!

(Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 29, 2023.)
Rais William Ruto wa Kenya akisalimiana na Balozi wa Japani nchini Kenya, Okaniwa Ken katika ikulu ya Nairobi,