Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Dr. Hawa Omari ambaye ni afisa kutoka Taasisi ya Elimu Maalum Kenya, (KISE) kuhusu kozi ya elimu jumuishi iliyoandaliwa nchini Japani na Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA) kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 30, 2023.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Dr. Hawa Omari akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala.
Dr. Hawa Omari akiwa na maafisa wengine kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria kozi kuhusu elimu jumuishi iliyoandaliwa na JICA na kufanyika nchini Japani.
Picha ya pamoja ya washiriki wa kozi ya elimu jumuishi kutoka nchi 17 iliyoandaliwa na JICA nchini Japani.