Ripoti: Darasa la kujifunza Kiswahili katika shule ya sekondari ya juu ya Keio Shiki
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu darasa la kujifunza Kiswahili linalofanyika katika shule ya sekondari ya juu ya Keio Shiki iliyopo mkoani Saitama nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 8, 2023.)
Darasa la kujifunza Kiswahili likiendelea katika shule ya sekondari ya juu ya Keio Shiki mkoani Saitama.
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Jonas Songora akimhoji mmoja wa wanafunzi wa Kiswahili.
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Jonas Songora akimhoji mwalimu wa darasa la Kiswahili Inoue Mayuko.