Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Yukizaki Lear anayeishi kisiwani Kyushu nchini Japani ambaye anatusimulia tajiriba yake ya miaka 25 ya kuishi nchini humo ikiwemo kufungua duka lenye bidhaa za asili za utamaduni wa Tanzania.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Yukizaki Lear akiwa na binti yake ambaye ni mwanamitindo.
Duka la Yukizaki Lear linaloitwa Kilimanjaro.
Bidhaa mbalimbali za asili ya Kitanzania katika duka la Yukizaki Lear.