Mahojiano: Yamamoto Mio
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na msikilizaji wetu wa siku nyingi Yamamoto Mio raia wa Japani ambaye anaelezea namna Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN ilivyomsaidia kujifunza lugha ya kiswahili.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Yamamoto Mio, Mjapani ambaye amekuwa akisikiliza Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN kwa miaka minne.