Mahojiano na Martin Mwanje na Riwaya ya “Chumba cha Kuogea Ndani ya Bahari” iliyoandikwa na Kumozome Yuu: Sehemu ya Kwanza
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na mwanahabari Martin Mwanje kuhusu hatua za kukabiliana na ukame katika maeneo yaliyoathirika na janga hilo nchini Kenya baada ya JICA kutoa msaada wa lori za maji, kisha utasikiliza riwaya ambapo mhusika mkuu amechoka kwa kusafiri na anaingia bila utaratibu maalum kwenye bafu ya umma iliyopo katika mji mdogo. Mashine ya tiketi ina majina yasiyo ya kawaida ambayo yanarejea vyumba vya kuoga vya kibinafsi. Akiwa kwenye mkanganyiko, anabonyeza kitufe kimoja na kuingia ndani, na kukutana na tukio la ajabu, tofauti na kitu chochote alichowahi kuona. Anajifanya kuwa si jambo jipya kwake na anajitosa kuoga bila kupata maelezo yoyote. Ameingia katika tukio lisilokuwa la kawaida.