Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mwanamke wa Kijapani Kato Reina kutoka mkoa wa Shizuoka nchini Japani aliyewahi kutembelea mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania na kuishi huko kwa miaka miwili akifanya kazi za kujitolea kama Afisa Maendeleo ya Jamii kupitia Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA).
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mwanamke wa Kijapani Kato Reina, akiwa amevalia vazi la khanga pamoja na mmoja wa wenyeji wake nchini Tanzania.