Riwaya: "Mwanga wa Kukaribisha" na Shigematsu Kiyoshi: Sehemu ya Pili
Kijiji kidogo kilichojificha kwenye bonde kina hadithi kuhusu kuwachukua watu ambao walishindwa katika vita hapo zamani za kale. Kwa sasa, kijiji hicho kimekuwa mahali pa kuwapokea watoto wasio na makazi na mahali pa kwenda.
Watoto hutembelea kijiji hicho wakati wa msimu wa joto kwa siku tatu mchana na siku mbili usiku ili kusaidia katika tukio linaloitwa "kuwakaribisha wadudu" ambalo linahusisha kuweka taa zaidi ya mia tatu kwenye njia za miguu katikati ya matuta ya mpunga. Tamaduni hiyo hapo awali ilifukuza wadudu wabaya kwa moto na moshi, lakini kijiji hiki kimegeuza kuwa tambiko la kuwakaribisha wadudu kwa mwanga. Watoto hutumia muda wao katika kijiji hiki ambacho kimejaa huruma. Je, ungependa kutembelea?