Mahojiano: Madinda Patrick Mwani
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Madinda Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania ambaye anatuelezea tajiriba yake ya mwaka mmoja akiwa nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Madinda Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa mwaka mmoja mjini Nagai mkoani Yamagata nchini Japani akiwa amevaa vazi lililotumika katika vita.
Madinda Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa mwaka mmoja mjini Nagai mkoani Yamagata nchini Japani akiwa na vazi la Kimono.
Madinda Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania ambaye amemaliza muda wake wa mwaka mmoja mjini Nagai mkoani Yamagata nchini Japani akikimbia na vazi la kimasai.