Mahojiano: Dorkasi Mwakawanga
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Dorkasi Mwakawanga, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Hiroshima nchini Japani kuhusu maarifa ya asili na tamaduni katika kukuza usalama na afya ya mwanamke wakati wa ujauzito na kujifungua.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Dorkasi Mwakawanga akiwa na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala.