Ripoti: Semina ya Tafiti za Afya na Masuala ya Afrika

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu Semina ya Tafiti za Afya na Masuala ya Afrika iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TKP uliopo Shimbashi jijini Tokyo nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Julai 30, 2023.)

Profesa Mirgissa Kaba, kutoka Kitivo cha Afya ya Umma katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Kyoto akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba shufaa katika kutimiza utoaji huduma ya afya kwa wote.
Dorkasi Mwakawanga, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Hiroshima akiwasilisha mada kuhusu maarifa ya asili na tamaduni katika kukuza usalama na afya ya mwanamke wakati wa ujauzito na kujifungua.
Harada Hidenori, ambaye ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Kyoto akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa maji safi na salama, matumizi ya vyoo, na kunawa mikono.