Mahojiano: Sakai Shinobu
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Sakai Shinobu raia wa Japani ambaye amecheza mpira wa kulipwa katika timu ya Geita Gold inayoshiriki ligi kuu nchini Tanzania. Ameweka rekodi ya kuwa Mjapani wa kwanza kucheza ligi hiyo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Sakai Shinobu akiwa mazoezini katika timu ya Geita Gold ya nchini Tanzania.
Sakai Shinobu akiwa mazoezini katika timu ya Geita Gold ya nchini Tanzania.
Sakai Shinobu akiwa na rafiki zake katika timu ya Kilimanjaro FC inayoundwa na Watanzania wanaoishi nchini Japani.