Ripoti: Maonyesho ya Tokyo ya Kukabiliana na Moto na Kujikinga na Majanga
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu Maonyesho ya Tokyo ya Kukabiliana na Moto na Kujikinga na Majanga.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala akiwa na Eugene Meshi raia wa Tanzania katika maonyesho hayo.