Mahojiano: Balozi Baraka Luvanda
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Balozi wa Tanzania nchini Japani, Baraka Luvanda kuhusu jitihada za ubalozi huo kufanikisha uuzwaji wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa maarufu nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Balozi wa Tanzania nchini Japani, Baraka Luvanda akiwa na kahawa ya Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Japani, Baraka Luvanda akiwa na viongozi wa migahawa maarufu ya uuzaji kahawa nchini Japani.
Baadhi ya kahawa ya Tanzania inayouzwa katika migahawa maarufu nchini Japani.
Baadhi ya kahawa ya Tanzania inayouzwa katika migahawa maarufu nchini Japani.