Mahojiano: Mhandisi Richard Munao Kanui
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mhandisi Richard Munao Kanui kutoka Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo nchini Kenya kuhusiana na mkutano ulioandaliwa na kituo cha AFICAT, kupitia Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa au JICA kuhusiana na matumizi ya mashine katika kilimo, uliofanyika jijini Tokyo, Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mhandisi Richard Munao Kanui kutoka Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo nchini Kenya.