Mahojiano: Shun Kojima
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mjapani, Shun Kojima ambaye anasimulia maisha yake alipokwenda kujifunza kiswahili na pia kushiriki mchezo wa soka katika timu ya ligi daraja la pili kisiwani Unguja nchini Tanzania.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Mei 28, 2023.)
Shun Kojima, raia wa Japani ambaye aliishi kisiwani Unguja nchini Tanzania na kushiriki mchezo wa soka katika timu ya daraja la pili.