Mahojiano: Mizouchi Yoshiyuki
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mjapani, Mizouchi Yoshiyuki ambaye amewahi kufanya kazi nchini Tanzania na Uganda ikiwemo kufundisha mchezo wa judo katika Chuo cha Polisi nchini Tanzania.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mizouchi Yoshiyuki akiwa na medali ilizopata timu ya taifa ya Judo ya Uganda katika mashindano ya Afrika Mashariki.
Mizouchi Yoshiyuki akiwa na mchezaji wa Judo wa Tanzania katika mashindano ya Dunia jijini Tokyo, Japani.
Mizouchi Yoshiyuki akiwa na wachezaji wa Judo wa Tanzania.
Mizouchi Yoshiyuki akiwa na wenyeji wake mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania.