Mahojiano: Hashim Abdi Hashim
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mtanzania Hashim Abdi Hashim anayefanya kazi katika kituo cha kutunza wazee nchini Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza! (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 14, 2023.)
Hashim Abdi Hashim, Mtanzania anayefanya kazi katika kituo cha kutunza wazee nchini Japani.