Ripoti: Hekaheka za mtaa wa Shibuya
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu mtaa maarufu jijini Tokyo, Shibuya ambao umekuwa kivutio kikubwa kwa vijana na watalii kutoka nje ya Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala akiwa na Watanzania wenzake katika mitaa ya Shibuya jijini Tokyo.