Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na mwanafunzi wa Kitanzania, Baraka Mkumbe anayesomea shahada ya uzamivu katika Sayansi ya Tiba kwenye Chuo Kikuu cha Tohoku nchini Japani.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Baraka Mkumbe, mwanafunzi kutoka Tanzania anayesoma katika Chuo Kikuu cha Tohoku nchini Japani.