Mahojiano: Takeda Nanae
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Takeda Nanae raia wa Japani anayefanya kazi katika ubalozi wa Japani nchini Tanzania ambaye pia aliwahi kufanya kazi za kujitolea katika hospitali ya mkoa wa Iringa nchini Tanzania.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Takeda Nanae raia wa Japani anayefanya kazi ubalozi wa Japani nchini Tanzania.