Ripoti: Uchaguzi wa viongozi wa Tanzanite Society
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu tunakuletea ripoti kuhusu uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Japani maarufu "TANZANITE SOCIETY" uliofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini Japani uliopo jijini Tokyo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Viongozi wa Tanzanite Society waliochaguliwa wakiwa na balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda (wa pili kutoka kulia).
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WOLD JAPAN, Mbozi Katala akiwa na wenzake Sabra Abdallah (kushoto) na Rahel Msuya (kulia).