Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu tunakuletea ripoti kuhusu kongamano lililopewa jina la "Kuelekea Maendeleo Endelevu kwa kuzingatia uwezo wa nchi za Afrika," lililofanyika katika chuo kikuu cha Utsunomiya nchini Japani mnamo Machi 8, 2023.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!