Mahojiano: Rugius Daniel Mtega

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Rugius Daniel Mtega ambaye yupo nchini Japani akishiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Utsunomiya kwa ushirikiano na vyuo vikuu 6 kutoka Barani Afrika.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!