"Bunju Arejesha Fadhila" iliyoandikwa na Tamaru Masatomo anayetambuliwa kama mwandishi anayeongoza wa hadithi fupi katika kizazi hiki. Hadithi hii kwa uwazi ina muundo mpya wa hadithi maarufu ya Kijapani "Korongo Arejesha Fadhila" inayohusu kijana anayeishi Japani ya sasa kama mhusika mkuu. Katika "Korongo Arejesha Fadhila," korongo aliyeokolewa na mwindaji anakuwa binadamu ili kulipa fadhila hiyo. Lakini hadithi inaisha kwa huzuni kwa korongo kuondoka baada ya mwindaji kuvunja mwiko kwa kuona umbo lake halisi. Toleo hili lina bunju. Ni namna gani bunju atakwenda kurejesha fadhila? Ni mwisho gani unamngoja mhusika mkuu aliyemwokoa samaki huyu? Furahia sauti ya simulizi yenye vionjo vya pop ambayo inaanzisha upya hadhithi kwa ustadi na mwisho unaojumuisha chaguzi za kisasa zilizofanywa na wanandoa wachanga.
Tamaru Masatomo, "Bunju Arejesha Fadhila"
(kutoka Chupa ya Rangi ya Bahari, Shuppan Geijutsusha)