Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Profesa Mshiriki Kurosaki Ryugo wa Chuo Kikuu cha Uchumi cha mji wa Takasaki nchini Japani.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Profesa Mshiriki Kurosaki Ryugo wa Chuo Kikuu cha Uchumi cha mji wa Takasaki nchini Japani.