Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mpelwa Sekela Nyanda, mmoja wa wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, anayeishi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita nchini Tanzania. Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mpelwa Sekela Nyanda, msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.