Mahojiano: Profesa Abe Yuko
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Profesa Abe Yuko, raia wa Japani anayefanya utafiti wa lugha ya Kibende inayozungumzwa nchini Tanzania katika maeneo ya mwambao wa ziwa Tanganyika. Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Profesa Abe Yuko