Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala akiwa ameshika barakoa na maharagwe ya soya ikiwa ni ishara ya tukio la kitamaduni la setsubun nchini Japani ambapo watu hurusha maharagwe ya soya kama ishara ya kumfukuza shetani wakati wa kuingia msimu mwingine.