Mahojiano: Kulwa Abel Jackson
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Kulwa Abel Jackson, Mtanzania anayeishi nchini Japani. Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Kulwa Abel Jackson akiwa katika shamba la maua, mkoani Yamagata nchini Japani.
Sehemu ya shamba la maua, kazi anayoifanya Kulwa Abel Jackson.
Kulwa Abel Jackson akiwa katika shimo la theluji akifurahia msimu wa baridi nchini Japani.