Mahojiano: Patrick Mwani
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania aliyepo mjini Nagai mkoani Yamagata nchini Japani. Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Patrick Mwani, mshauri wa michezo kutoka nchini Tanzania aliyepo mjini Nagai, mkoani Yamagata nchini Japani.