Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na msikilizaji wa siku nyingi wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WOLRD JAPAN, Mchana J. Mchana kutoka Morogoro nchini Tanzania. Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Mchana J. Mchana, msikilizaji wa muda mrefu wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WOLRD JAPAN.