Mahojiano: Wanariadha kutoka Tanzania
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, wageni wetu ni wanariadha kutoka Tanzania ambao Oktoba 16 walishiriki mbio za Nagai Marathon mwaka 2022. Mbio hizo zilifanyika ikiwa ni mwendelezo wa diplomasia ya michezo na kushirikisha wanariadha kutoka Tanzania na Japani wapatao 800.
Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni tu baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Wanariadha wa Tanzania walioshiriki mbio za Nagai Marathon 2022, kutoka kulia ni Fabian Naasi, Ezekiel Ngimba, Angelina Yumba, kiongozi wao Juma Ikangaa, Alphonce Simbu na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala.
Mwanariadha Alphonce Simbu akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN.