Mahojiano: Leonard Zimbehya (Kachebonaho).
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, mgeni wetu ni Leonard Zimbehya maarufu Kachebonaho, mkulima wa kahawa kutoka nchini Tanzania ambaye anaelezea faida za ushiriki wake katika Mkutano na Maonyesho ya SCAJ ya Utaalam wa Kahawa Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika nchini Japani katika ukumbi wa Tokyo Big Sight kuanzia Octoba 12 hadi 14.

Maonyesho hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Wataalam wa Kahawa nchini Japani (SCAJ). Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni tu baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Leonard Zimbehya maarufu Kachebonaho (kushoto), akiwa na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN, Mbozi Katala.
Leonard Zimbehya maarufu Kachebonaho akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD JAPAN..
Washiriki wa Mkutano na Maonyesho ya SCAJ ya Utaalam wa Kahawa Duniani mwaka 2022 kutoka Tanzania wakiwa katika banda lao katika ukumbi wa Tokyo Big Sight.
Bango la Mkutano na Maonyesho ya SCAJ ya Utaalam wa Kahawa Duniani mwaka 2022 katika ukumbi wa Tokyo Big Sight.