Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu "Kuleta Mabadiliko Duniani Kupitia Michezo". Mjadala uliohusisha wanamichezo kutoka Japani na mwanariadha kutoka Sudan. Tukio hilo liliandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Global Festa Japan, kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani, Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (JANIC). Usikose kusikiliza!
Washiriki wa mjadala kuhusu "Kuleta Mabadiliko Duniani Kupitia Michezo", wakiwa katika tukio la Global Festa Japan lililofanyika Oktoba Mosi na Pili.
Mchezaji mstaafu wa timu ya taifa ya ragbi ya Japani, Hirose Toshiaki.
Mwanariadha mstaafu wa Japani, Yokota Masato ambaye kwa sasa ni kocha wa mwanariadha wa Sudan, Abraham Guen.