Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu tukio la ushirikiano wa kimataifa kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu hali ya sasa na hitaji la ushirikiano wa kimataifa. Tukio hilo limeandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Global Festa Japan, kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani, Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali. (JANIC). Usikose kusikiliza!
Wachekeshaji Suehirogarizu (waliovaa kitamaduni) na ODA Man wakitoa burudani katika tukio la Global Festa Japan.
Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD-JAPAN, Mbozi Katala akiwa katika tukio hilo.
Wafanyakazi wa kujitolea raia wa Japani wakiwa katika banda lao la KESTES, hukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia ufadhili wa masomo kwa watoto nchini Kenya.
Balozi wa Malawi nchini Japani, Kwacha Chisiza (katikati), akiwa na maafisa wa ubalozi huo pamoja na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WORLD-JAPAN, Mbozi Katala kwenye banda la ubalozi huo.