Mahojiano: Balozi Baraka Luvanda
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, mgeni wetu ni Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda ambaye anaelezea faida za Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika, TICAD 8, kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni tu baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!