Ripoti: Kuwasimulia Watoto kuhusu Afrika
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Pia tunakuletea ripoti za kila aina, na wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu tukio aliloshiriki mwanamuziki Anyango kwenye shule moja ya msingi nchini Japani. Mwanamuziki huyo anafahamika sana kutokana na upigaji wake stadi wa ala ya nyatiti. Usikose kusikiliza!
Anyango akiwatumbuiza wanafunzi kwa kupiga ala ya nyatiti.
Anyango akijibu maswali ya wanafunzi.